Mtakatifu (Holy) by Frank Njuguna

Leave a comment(Sung in Swahili)

Sitaabudu miungu mingine, (I will not worship other gods)
Iliyo na mifano yeyote (Fashioned in any way)
Sitapiga magoti yangu nisujudu (I will not bow down to worship)
Nitakusanya sadaka zangu ziwe manukato (But will bring my offering as incense)
Kwa Yesu, astahili sifa (To Jesus, who deserves praise)

Chorus:
Naleta sadaka za sifa kwako Bwana (I bring my sacrifice of praise to You Lord)
Heshima na mamlaka zipokee (Receive all the glory and honor)
Mtakatifu, mtakatifu, nakuita mtakatifu (Holy, Holy, I call you Holy)
Oh Yesu, wewe mtakatifu (Oh Jesus, You are Holy)

Pokea sifa na utukufu (Receive praise and glory)
Na heshima ni zako Bwana (And all honor belongs to you Lord)
Pokea sifa na utukufu (Receive praise and glory)
Na heshima Bwana (And honor, Lord)

Bridge:
Uh, Oh Yesu, wewe mtakatifu (Uh…, Oh Jesus you are Holy)

Shuka Baba (Come Down Father) Lyrics by Eunice Njeri

Leave a comment(Sung in Swahili)

Shuka utende Yesu, Kenya tunakungoja (Come down Jesus, Kenya awaits you)
Shuka utende Yesu, Watu tunakungoja (Come down Jesus, we are waiting for you)

Refrain:
Hapa hatutoki Bwana, hadi tukuone (We won’t leave, until we see you)
Wala hatutasinzia, hadi tukuone (Neither shall we slumber, until we see you)
(Shuka ee, Shuka Baba – (Come down, Come down Father))

Jamii zilizotengana, mayatima Baba (Conflicted tribes and the orphans father)
Viumbe vyote Baba, wote tunakungoja (All creations Father, we all await)
Jamii zilizotengana, mayatima Baba (Conflicted tribes and the orphans father)
Nena neno moja, wote tunakungoja (Just say one word, we are all waiting for you)

(Refrain)

Wajane na wagonjwa, matajiri wote (The widows, the sick and the rich)
Dunia nzima yahweh, wote tunakungoja (All the world awaits you Yahweh)
Nena kwa sauti, nena neno lako (Speak with a loud voice, speak your word)
Tu tayari kusikiza, wote tunakungoja (We are ready to listen, we all await you)

(Refrain)

Bridge:
Kama siku, siku ya Pentekote (Just like the day of Pentecost)
Shuka na moto wako, ututembelee  (Descend with your fire, and visit with us) (Repeat)

(Refrain)

Mwanake (His Son) Lyrics by Benachi Ft. Kaberere

Leave a comment(Sung in Swahili)

Usinione nimechakaa unitilie dharau (Don’t look at my tatters and despise me)
Mimi binadamu, umesahau? (I am also human, have you forgotten?)

Unaishi kwa dhamani, (You live in riches)
Mimi naishi kwa imani (I live on faith)
Mbele zako mimi sina haki, (Before you I have no rights)
Mbele zake mimi mwenye hadhi (But before Him, I am valuable)
Fahamu kuwa Mola ndiye aliniumba mimi na wewe (Remember God is the creator of all)

Refrain:
Mimi mwanake, usiku nitalala (I am His son, I will sleep in peace)
Mbele zake maulana, sote tuko sawa (For before the Lord, we are all equal)

Ulinipuuza mie, eti sifai kuwa nawe (You wrote me off as useless)
Uliniona mie, eti hati ya kula nawe (I was not worthy to eat with you)
Sahani moja tupotiliwa chakula (From one plate when we were served)
Nyumba moja tulipofaa kuishi pamoja (In one house as we were meant)

(Refrain)

Wema wake taji la upendo juu yangu (His love and mercy are my crowns (?))
Ndani yake nilikuwa na uwoga wote uwe kimya (Before Him, all my fears are silent)

(Refrain)

Ni Wewe (It’s You) Lyrics by Janet Otieno

1 Comment


(Sung in Swahili)

Naomba uniweke kwako ndani (I pray that you keep me in You)
Niwe imara kama milima Zayuni (That I may be strong like Mount Zion)
Hauta anguka kukiwa na mawimbi (That will Neither be fallen by storms)
Wala kutikiswa kukiwa na adui (Nor be shaken by enemies)
Kila kitu ni wewe (Everything is you)

Refrain:
Kila kitu changu ni wewe (Everything that is mine, is yours)
Ninaye mwimbia, ni wewe (The one I praise, is you)
Maishani mwangu, nimeamua ni wewe (In all my life, I have decided that It’s you)

Mi nimeshangazwa na matendo yako Baba (I’m amazed by your works Father)
Ulivyonichukua na kunitunza kama wako (The way you took me and made me yours)
Sa mi ni wako, Kwangu kwako (Now I am yours, what is mine is yours)
Ukanipenda, ukaniita mwana wako (You loved me, and called me your son/child)

(Refrain)

Juu, chini, kushoto kulia (Up or down, left or right)
Sijamwona kama wewe (I have not seen anyone like you)
Sa mi ni wako, Kwangu kwako (Now I am yours, what is mine is yours)
Ukanipenda, ukaniita mwana wako (You loved me, and called me your son/child)

(Refrain)

Muziki ni Dawa (Music Heals) Lyrics by Ringtone Apoko

Leave a comment(Sung in Swahili)

Refrain:

Asante kwa muziki, asante Mungu kwa ngoma (Thank you, Thank you God for music)
Hebu wewe ona vile watu wako wanapona (Look at how Your people sing & are healed)
Muziki ni dawa, ukisikiza utakuwa sawa (Music heals, listen to it and be eased)
Muziki ni dawa, ndio maana mimi naimba (Music heals, and that is why I sing)

Shida zinanionea, maisha ni kuvumilia (My life is full of troubles, I try to persevere)
Mimi nang’angana ili (…) I’m working hard (I work hard that…)
Mwili waanza kuuma kichwa kinaniuma (My body starts to ache, I have a headache)
Mgongo unauma, madawa nanywa siponi (My back aches, No medicine works)
Nasikia muziki kwa redio, mwili wangu unapoa (I listen to radio music, my body eases)
Swali munijibu: huu muziki una nini? (Answer me this: What does music have?)

(Refrain)

Nilikuwa nimepewa stori ya mfalme mmoja (I was told a story about a king)
Kwa jina aliitwa Sauli, alipagawa mwili (His name was Saul, and he was possessed)
Kulikuwa na kijana mmoja, kwa jina Daudi (There was a young man called David)
Alikuwa na talanta, talanta kama mimi (He had a talent, a talent similar to mine)
Tofauti yangu mimi na yeye, Ye alicheza zeze (The difference was he played the harp)
Mfalme alipagawa, watu wakashtuka (People were afraid whenever the King was ill)
Madakitari waliitwa kutibu mfalme wakashindwa (Healers tried to heal him in vain)
Daudi alipocheza zeze, mfalme akapona (But when David played the harp, the king was eased)

(Refrain)

Older Entries

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,353 other followers

%d bloggers like this: